Manchester United’s Champions League heartbreaker Luka KIUNGO Luca Modric bado ana moyo wa kutaka kujiunga na Mashetani Wekundu wa Old Trafford.
Nyota huyo wa Real Madrid aliwafungia bonge la bao mabingwa hao wa Hispania wakifunga United katika usiku wa utata kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita.
Sasa imebainika kuwa, kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia mwenye umri wa miaka 27, bado ana ndoto za kurejea kucheza Ligi Kuu ya England katika kikosi cha United.
Bao la Luka Modric liliiwezesha Real Madrid kuitoa Manchester United
Modric alikuwa anatakiwa kwa udi na uvumba na kocha wa United, Sir Alex Ferguson misimu miwili iliyopita akachukue nafasi ya Paul Scholes. Lakini United ilikwama kumsajini mchezaji huyo baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, ambaye walitibuana juu ya biashara ya Dimitar Berbatov mwaka 2008.
Modric baadaye akaondoka White Hart Lane kwenda Real kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 33 msimu huu, lakini amekosa namba ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Jose Mourinho na bao alilofunga Old Trafford wiki iliyopita lilikuwa ni la pili kwake katika msimu mgumu.