KIUNGO Jack Wilshere anaweza kuzikosa mechi ngumu za England kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya San Marino na Montenegro.
Kiungo huyo tegemeo wa Arsenal, ataikosa pia mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya timu yake ikienda Ujerumani kumenyana na Bayern Munich, kutokana na kuchelewa kupona maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati wakilala 2-1 mbele ya Spurs siku tisa zilizopita.
Hatakuwamo katika kikosi kinachosafiri kwenda Bavaria leo na hatarajiwi kupona hadi kufika Jumamosi katika mechi nyingine na Swansea.
Jack Wilshere anapambana kuwa fiti kwa ajili ya kuichezea England dhidi ya San Marino na Montenegro