• HABARI MPYA

    Thursday, June 13, 2013

    BABU MFARANSA AREJEA NA KUSEMA; "NIPO KAZINI SIMBA HADI MWEZI WA SITA MWAKANI"

    Kocha Liewig (katikati) wakati anawasili nchini kwa mara ya kwanza kuja kufanya kazi Simba SC. Kushoto ni Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala akimpokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Januari mwaka huu
    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 13, 2013 SAA 8:50 MCHANA
    KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig ametua leo nchini na kusema anatambua bado yuko kazini hadi Juni mwakani, ingawa amekiri klabu hiyo kuajiri kocha mwingine, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY mida hii, Liewig amesema kwamba hajafukuzwa Simba SC bali alikwenda kwao Ufaransa kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    “Nilipoondoka hawakusema wanaachana na mimi, waliniambia nakwenda kupumzika, na vitu vyangu vyote niliacha hotelini. Kama wangesema mimi basi, nisingerudi hapa. Sitaki matatizo na mtu, ningebaki tu nyumbani,”alisema.
    Hata hivyo, Liewig alisema amekwishanzumgza na Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage na ameahidi kukutana naye mwisohoni mwa wiki kutatua tatizo lake.
    “Nitakutana na Rage mwishoni mwa wiki kuzungumza, sitaki matatizo na wao, wanilipe haki zangu kwa mujibu wa Mkataba wetu mimi nitaondoka,”alisema. 
    Liewig akisaini Mkataba na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' Januari mwaka huu mjini Dar es Salaam.

    Alipoulizwa kama baada ya kuwasili ataanza kazi, Liewig alisema; “Ngoja kwanza nikutane na Rage, namuheshimu na baada ya kuzungumza naye nitajua,”alisema.
    Liewig alisani Mkataba wa mwaka mmoja na nusu Januari mwaka huu kuifundisha Simba SC akirithi mikona ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago.     
    Katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo kwa miezi mitano, Liewig aliiongoza Simba katika mechi 25 akiiwezesha kushinda tisa, sare nane na kufungwa saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BABU MFARANSA AREJEA NA KUSEMA; "NIPO KAZINI SIMBA HADI MWEZI WA SITA MWAKANI" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top