• HABARI MPYA

    Tuesday, June 11, 2013

    CHELSEA ITAKULA 'ZA USO' TU KWA ROONEY, SERA YA MAN UNITED HAIRUHUSU KLABU KUUZA MCHEZAJI KWA WAPINZANI ENGLAND

    IMEWEKWA JUNI 11. 2013 SAA 8:50 MCHANA
    MPANGO wa Jose Mourinho kumsajili Wayne Rooney unaweza kuvurugwa na sera ya Manchester United kutouza wachezaji wake kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya England.
    Kocha mpya wa Chelsea, Mourinho aliweka wazi juu ya mpango wa kuvamia Old Trafford kwa mpinzani wake, David Moyes wiki hii kwa kusema kwenye Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari tangu arejee Stamford Bridge kwamba Rooney lazima ajiulize kipi kitamfanya awe na furaha.
    Ombi lolote rasmi kutoka klabu hiyo ya London juu ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 litakutana na jibu ‘hapana’ kutoka kwa Moyes na Mtendaji Mkuu mpya wa United, Ed Woodward.
    United imekuwa na sera hiyo kwa muda mrefu kutouza wachezaji wake nyota kwa wapinzani wao England. Ikiwa wachezaji wanasistiza kuondoka kama David Beckham na Cristiano Ronaldo walivyofanya – huuzwa kwa klabu nyingine barani Ulaya.
    Mchezaji mmoja – beki Mikel Silvestre – aliuzwa Arsenal na kocha aliyetangulia United, Sir Alex Ferguson mwaka 2008, lakini Mfaransa huyo wakati alikuwa amechuja.
    Ferguson alipambana vikali kumzuia beki wa kushoto wa Argentina, Gabriel Heinze kujiunga na Liverpool mwaka uliotangulia, ambaye alihamia Real Madrid.
    Should he stay or should he go: United have used Rooney on posters advertising the home kit for next season
    Abaki au aondoke: United imemtumia Rooney mabango ya matangazo ya jezi za nyumbani msimu ujao

    Rooney anatarajiwa kurejea United kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Julai 3 na hadi sasa hakuna dalili kwamba hatatokea. Pia anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya Australia na Asia Julai 10.
    BIN ZUBEIRY iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba nyota huyo wa zamani wa Everton alimuomba Ferguson kuondoka United, lakini inafahamika matatizo ya mshambuliaji huyo yalikuwa dhidi ya kocha huyo wa zamani– ambaye aliamua kumuweka benchi katika kila mechi kubwa. 
    Moyes na Rooney wanatarajiwa kukutana kwa mazungumzo kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA ITAKULA 'ZA USO' TU KWA ROONEY, SERA YA MAN UNITED HAIRUHUSU KLABU KUUZA MCHEZAJI KWA WAPINZANI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top