IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 9:14 ALASIRI
MSHAMBULIAJI Iago Aspas anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 7.5 kutua Liverpool baadaye leo, baada ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Mpachika mabao huyo wa Celta Vigo, ambaye amefunga mara 12 katika La Liga msimu uliomalizika, ameahirisha kwenda mapumzikoni ili kutua Anfield kukamilisha mazungumzo na Wekundu hao.
Aspas, mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliwasili England jana usiku, alisema: "Nimelazimika kuahirisha safari yangu ya mapumziko Caribbean, lakini sababu ya kufanya hivi naweza kufafanua kwa nini. Wakati niliposikia Liverpool wananitaka sikusita hata kwa dakika moja.'
Suti na buti: Iago Aspas anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 7.5 kutua Liverpool leo
Karibu Merseyside: Iago Aspas amewasili Liverpool
"(Liverpool) ni moja ya klabu kubwa duniani na nafikiri nilikuwa nina ofa pia kutoka Italia na Ureno na nchi nyingine, nikaamua mustakabali wangu ni katika soka ya England,"alisema.
Klabu hiyo ya Merseyside imekubali kutoa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7.5 kwa mtumia guu la shoto huyo ambaye ataomba msaada wa wachezaji wenzake kujifunza Kiingereza.
"Natumai nitapata msaada kutoka kwa (Jose) Reina, Suso, Dani Pacheco, Luis Suarez, (Philippe) Coutinho, Lucas Leiva na Jose Enrique,"alisema.