• HABARI MPYA

    Friday, June 14, 2013

    DILI LA RONALDO KUREJEA MAN UNITED LARUDI UPYA...MWENYEWE AKANA KABISA KUSAINI MKATABA MPYA REAL

    IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 2:30 ASUBUHI
    MPANGO wa Cristiano Ronaldo kurejea Ligi Kuu ya England sasa uhai tena baada ya mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 80 kukanuisha taarifa za kusaini Mkataba mpya Real Madrid.
    BIN ZUBEIRY iliandika mwezi uliopita, kwamba Manchester United inajiamini itamsajili tena mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, Ronaldo kabla ya taarifa kutolewa kwa umma kwamba yuko tayari kusaini Mkataba mpya kubaki Bernabeu kwa kipindi chake chote kilichobaki kwenye soka.
    Unsettled: Ronaldo told the 58million people who like his page on Facebook about his situation
    Aliyepepesuka: Ronaldo amewaambia ukweli wake watu Milioni 58 walio like ukurasa wake wa Facebook
    Unsettled: Ronaldo told the 58million people who like his page on Facebook, about his situation
    Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alisema mapema wiki hii kwamba alikuwa anajiamini mchezaji huyo atasaini Mkataba wa kuendelea kuichezea Real, akisema: "Lengo langu, lengo la Cristiano, na lengo la mashabiki wote wa Real Madrid ni kwamba anaendelea kucheza hapa kwa miaka mingi ijayo.’
    Pamoja na hayo, akitumia ukurasa wake wa Facebook na akaunti yake ya Twitter, Ronaldo, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa, alisema: "Habari zote kuhusu kusaini kwangu Mkataba mpya Real Madrid ni uzushi,".
    In demand: Any club in the world would want a player of Ronaldo's ability after his spells at United and Madrid
    In demand: Any club in the world would want a player of Ronaldo's ability after his spells at United and Madrid
    Dhahiri klabu yoyote duniani ingetaka kunufaika na uwezo wa Ronaldo baada ya kuzitumikia United na Madrid.
    Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo unamalizika mwaka 2015, lakini amegoma kusaini mpya, Madrid haitakuwa na chaguo lingine zaidi ya kumuuza, ingawa ameunfga mabao mengi kupita kiasi,146 katika mechi 135.
    Monaco ilikuwa inaaminika kujiandaa kutoa Pauni Milioni 85 na kumshawishi kwa mshahara babu kubwa ajiunge nao, lakini Ronaldo anaweza kuchagua kurejea Manchester, ambako ameacha kumbukumbu.
    Alex Ferguson alikuwa anafikiriwa kuchangia kwa kiasi kikubwa Ronaldo kutorejea katika klabu hiyo, lakini anaweza kuwa na nia ya kwenda katika klabu hiyo ambayo ilimjenga na kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa duniani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DILI LA RONALDO KUREJEA MAN UNITED LARUDI UPYA...MWENYEWE AKANA KABISA KUSAINI MKATABA MPYA REAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top