IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 2:58 ASUBUHI
KLABU ya Manchester City imeipiga bao Chelsea katika mbio za kuwania saini ya Edinson Cavani baada ya mama wa mchezaji huyo kusema kwamba mwanawe amekwishaanza mazungumzo na viongozi wa Etihad.
KLABU ya Manchester City imeipiga bao Chelsea katika mbio za kuwania saini ya Edinson Cavani baada ya mama wa mchezaji huyo kusema kwamba mwanawe amekwishaanza mazungumzo na viongozi wa Etihad.
Mshambuliaji huyo wa Napoli anayeuzwa kwa Pauni Milioni 53, City inapambana na inaamini itaipata saini yake ili inufaike na huduma zake chini ya kocha mpya, Manuel Pellegrini.
Jose Mourinho anataka pia kumnasa mshambuliaji huyo wa Uruguay atue Stamford Bridge, lakini mtu hata mmoja katika klabu hiyo aliyezungumza na mchezaji huyo na Real Madrid tayari imeanza mipango ya kukinasa kipaji hicho moto Ulaya.
Hapa, kule, popote: Nyota huyu wa Uruguay ni mmoja kati ya wachezaji wanaosakwa kwa udi na uvumba Ulaya majira haya ya joto
Cavani, mwenye umri wa miaka 26, ameshinda kiatu cha dhahabu Serie A msimu uliopita kwa mabao yake 29 kwenye mechi 34, na pia akafunga mabao saba katika Europa League.
Mama yake, Berta Gomez ameiambia Redio ya Uruguay: "Edi anazungumza na Madrid na City. Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis, amezungumza na Chelsea lakini hakuna lolote. Ndani ya siku 15 au 20 tutajua anapokwenda.’