IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 3:10 ASUBUHI
KLABU ya Marseille imethibitisha nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayechezea Arsenal, Gervinho ambaye ametua jana Dar es Salaam na timu yake ya taifa kwa ajili ya mechi na Tanzania Jumapili.
Rasta huyo mwenye umri wa miaka 26, aliigharimu Arsenal Pauni Milioni 11 aliposajiliwa kutoka Lille na amekutana na wakati mgumu katika Ligi Kuu ya England.
Kocha Msaidizi wa Marseille, Franck Passi amesema: "Huu ni wasifu ambao unatuvutia, ndiyo. Tunataka wachezaji wa pembeni, wenye uwezo wa kuchezea mpira, kutoa pasi na kufunga na Gervinho ana wasifu huu,".
Benchi: Gervinho ameonyesha uwezo, lakini hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza Arsenal
Tangu asaini Arsenal mwaka 2011, Gervinho ameifungia mabao 11 klabu hiyo ya Kaskazini mwa London, machache mno ukilinganisha na winga mwenzake, Theo Walcott aliyefunga mabao 32 katika muda huo.
Na Arsene Wenger akiwa tayari kutumia kiasi cha Pauni Milioni 70 katika pazia la usajili, Gervinho pengo lake linaweza kuzibwa na mchezaji wa bei kubwa, kama nyota wa Fiorentina, Steven Jovetic au Gonzalo Higuain wa Real Madird.
Gervinho anaweza kuporomoka zaidi msimu ujao kutokana na Alex Oxlade-Chamberlain kutarajiwa kupewa nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza.
Barafu iliyoyeyuka: Wenger amempasha Gervinho wazi kwa kiwango cha chini kilichomkatisha tamaa