IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 1:16 USIKU
KOCHA Manuel Pellegrini hatimaye ameteuliwa kuwa kocha wa Manchester City kwa Mkataba wa miaka mitatu na amesema kikosi chake kipya kitakuwa bora katika ligi.
Amewasili kutoka Malaga na kuchukua nafasi ya Roberto Mancini aliyefukuzwa baada ya matokeo mabaya msimu uliopita.
Pellegrini amesema: "Nina furaha kukubali nafasi hii kubwa ya kuvutia. Klabu ina dira thabiti ya mafanikio ndani na nje ya Uwanja na ninajifunga kutoa mchango wangu muhimu,"alisema.
Tayari kwa kazi: Manuel Pellegrini amesema Man City ina kikosi bora katika Ligi Kuu ya England