IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
KLABU ya Manchester United imeongeza hali ya kujiamini kwamba wanaweza kuwapata wachezaji Cesc Fabregas na Robert Lewandowski wakatua Old Trafford majira haya ya joto.
Kocha mpya wa United, David Moyes angependa kuwasajili wote, kiungo wa Barcelona na mshambuliaji wa Kipoland wa Borussia Dortmund katika klabu yake kabla ya kikosi chake hakijakwenda katika ziara ya Asia na Australia katikati ya mwezi ujao.
Inafahamika kwamba, wachezaji wote hao wameonyesha nia zao za kuhamishia cheche zao kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England, hivyo United wanaweza kufanikisha dili hizo.
Man United wanaamini wanaweza kumnasa Cesc Fabregas na Robert Lewandowski (chini)
Robert Lewandowski
Klabu yake ya zamani Fabregas, Arsenal haijaonyesha kuwa tayari kumsajili tena iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ataondoka Nou Camp, lakini United inafahamika wanamtaka kwa dhati kiungo huyo aliyeichezea kwa miaka nane timu hiyo ya London kabla ya kurejea Hispania miaka miwili iliyopita.
Lewandowski anaweza kuhamia England baada ya matumaini yake kuhamia kwa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich kukatwa wiki hii.
United wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji huyo wa Poland kwa miezi kadhaa na wanaamini anaweza kuzalisha ushindani mzuri kwa Robin van Persie, ambaye atatimiza miaka 30 muda mfupi kabla timu haijaanza kutetea ubingw awake Agosti.
Changamoto: Robin van Persie anaweza kukabiliana na changamoto kubwa mwanzoni mwa msimu ujao Man United
Kuwasili kwake pia kunaweza kukuza shinikizo kw Wayne Rooney, ambaye ameomba kuondoka Old Trafford tangu mwishoni mwa msimu uliopita.


.png)