Mourinho akizungumza na Waandishi wa Habari wapatao 250 na alipoulizwa bado Special One, akajibu: "Mimi Happy One. Nina furaha sana.
Familia ya furaha: Mourinho akiwa na Mwenyekiti Bruce Buck (kushoto) na Mtendaji Mkuu, Ron Gourlay (kulia)
IMEWEKWA JUNI 10, 2013 SAA 3:50 USIKU
Jose Mourinho leo ametambulishwa rasmi kuwa kocha wa Chelsea kwa mara ya pili akirejea Stamford Bridge.
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari, aliambatana na benchi lake la ufundi, je unawajua?
Katika utambulisho: Kutoka kushoto, Rui Faria, Silvino Louro, Jose Morais, Steve Holland na Gary Staker katika Mkutano na Waandishi wa Habari wa kutambulishwa Jose Mourinho leo.
MOURINHO AMERUDI
Angalia Mkutano na Waandishi wa Habari wa kutambulishwa Jose Mourinho kurejea Chelsea HAPA
1. RUI FARIA
Faria ni mtaalamu wa ufiti wa wachezaji fambaye amekuwa akifanya kazi na Mourinho kwa miaka mingi.
Baada ya kukutana na Faria Barcelona, Mourinho alimuomba awe kocha wake wa ufiti atakapokuwa kocha wa Uniao de Leiria nchini Ureno.
Faria alifanya kazi na Mourinho Porto, mara ya yake ya kwanza Chelsea, Inter Milan na Real Madrid.
2. SILVINO LOURO
Louro ni kocha wa makipa mwenye uzoefu wa juu ambaye amekuwa sehemu ya benchi la ufundi la Mourinho tangu Porto.
Louro amewahi pia kuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Ureno. Amechangia kwa kiasi kikubwa ubora wa Petr Cech.
3. JOSE MORAIS
Morais ni mtu pekee mpya katika benchi la ufundi la Mourinho, ambaye hakufanya kazi na Chelsea kabla. Alifanya kazi na Mourinho kwa mara ya kwanza Porto kabla ya kuungana na Mreno huyo tena Inter Milan.
Morais kisha alifanya kazi kwa miaka mitatu na Mourinho Real Madrid kabla ya kujiunga na Chelsea.
4. STEVE HOLLAND
Holland aliiongoza timu ya wachezaji wa akiba wa Chelsea kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 2011 kabla ya kuhamia kikosi cha wakubwa. Awali alifanya kazi chini ya Andre Villas-Boas na kisha Roberto Di Matteo.
Kabla ya kujiunga na Chelsea mwaka 2009, Holland amefanya kazi miezi mitano katika akademi ya Stoke kama Mkurugenzi.
5. GARY STAKER
Staker Ofisa Mratibu wa Chelsea, ambaye awali aliajiriwa kama mkalimani wa timu wakati wa Claudio Ranieri kwa sababu alikuwa anajua Kitaliano.
P.S. unaikumbuka hii?
Benchi la Ufundi la Mourinho alipotambulishwa mara ya kwanza kuwa kocha wa Chelsea mwaka 2004.
Sura hizi: Kutoka kushoto, kocha wa Ufiti, Rui Faria, Jose Mourinho, Andre Villas-Boas, kocha wa makipa, Silvino Louro na Kocha Msaidizi, Steve Clarke na Baltemar Brito wakati Mourinho alipotambulishwa mara ya kwanza kuwa kocha wa Chelsea mwaka 2004. Villas-Boas baadaye alikuwa Kocha Mkuu wa Chelsea, lakini akatimuliwa ndani ya msimu mmoja.


.png)