IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 3:24 USIKU
BEKI wa pembeni, Guillermo Varela amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes.
BEKI wa pembeni, Guillermo Varela amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes.
DIli la kumsaini beki huyo mwenye umri wa miaka 20 wa kikosi cha Uruguay cha vijana chini ya umri wa miaka 20, kutoka klabu ya Penarol lilithibitishwa wiki iliyopita na amewasili Manchester kumwaga wino kwa mkataba wa miaka mitano leo.
Guillermo Varela akiwa na jezi ya Manchester United baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano
Guillermo Varela amejiunga na Manchester United wakati David Moyes akianza mapinduzi Old Trafford
"Nimefurahi sana kuwa sehemu ya klabu hii, moja ya timu bora duniani,"alisema Varela. Varela alifanya majaribio kwanza Old Trafford katika wiki za mwisho za msimu uliopita alivutia kiasi cha kuishawishi klabu iilipe Penarol Pauni Milioni 1.
Varela akisaini Mkataba wa miaka mitano
Guillermo Varela ni nani?
Alizaliwa Machi 24, mwaka 1993, mjini Montevideo, Uruguay
Aliichezea mechi ya kwanza Penarol Juni 2011, na haikuchukua muda akawa mchezaji wa kikosi cha kwanza katika beki ya kulia
Ameichezea mechi 10 timu ya taifa ya vijana ya Uruguay chini ya umri wa miaka 20, lakini bado hajachezea timu ya wakubwa
"Kama ambavyo kila mmoja duniani anafahamu, hii ni klabu kubwa ambayo imeshinda kila kitu na kwa kweli ninatumai kuendelea hivyo,".
"Nina bahari sana kuna watu wachache wanaozungumza Kispanyola hapa. Itanisaidia kutulia na kuweka mambo yangu sawa.'
Varela muda si mrefu ataungana na U20 ya Uruguay kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA la vijhana wa umri huo nchini Uturuki.
VIDEO: Varela akifanya vitu
Kocha mpya: David Moyes atakuwa na Varela Manchester United