IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 7:00 MCHANA
UTATA umetawala juu ya jezi mpya za Newcastle kutoka kwa wadhamini wao kutokana na mshambuliaji wake nyota, Papiss Cisse kujiandaa kukataa kuvaa tangazo la Wonga.com.



UTATA umetawala juu ya jezi mpya za Newcastle kutoka kwa wadhamini wao kutokana na mshambuliaji wake nyota, Papiss Cisse kujiandaa kukataa kuvaa tangazo la Wonga.com.
Mshambuliaji huyo wa Senegal ni muumini safi wa dini ya Kiislamu na aliwaada viongozi wa klabu hiyo juu ya kutokuwa tayari kwenda kinyuma cha maadili ya dini yake kwa kutangaza biashara za kampuni hiyo ya mikopo.
Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, waumini wa dini hiyo hawaruhusiwi kunufaika au kujinufisha na riba kutoka kwa mtu mwingine. Benki za Kiislamu hazitoi riba.
Siyo kwangu: Papiss Cisse atakataa kuvaa jezi za wadhamini, Wonga
Jezi za ugenini: Steven Taylor akiwa na jezi ya kampuni hiyo ya mikopo kwa riba
Wachezaji wenzake CIsse, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa, ambao pia ni Waislamu, nao pia wanaweza kugoma kuvaa jezi hizo.
Newcastle haiko tayari kuachana na mchezaji huyo na wanaweza wakafanya kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Tottenham na West Ham, Freddie Kanoute.
Mmali huyo aligoma kuvaa jezi ya nembo ya tovuti ya 888.com alipokuwa Seville miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya kamari.
Kanoute alishikilia msimamo wake na hakuvaa nembo hiyo kwenye mashindano ya Hispania, ingawa mazoezini alikubali kuvaa.
Baadaye alikubali kuvaa kwa masharti ya kutotumika katika matangazo yoyote ya kibiashara.
Wonga, ambao udhamini wao wa miaka minne unaanza msimu ujao, tayari inakabiliwa na zengwe lingine katika masuala ya utozaji wa riba za mikopo yake.
Frederic Kanoute aligoma, baadaye akakubali kuvaa jezi ya wadhamini 888