• HABARI MPYA

    Wednesday, December 12, 2012

    ATUDO AANGUKA MIWILI AZAM FC

    Atudo

    Na Mahmoud Zubeiry
    BEKI wa kimataifa wa Kenya, Joackins Atudo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
    Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa amesema mida hii kwamba, beki huyo kutoka Tusker ya Kenya, amekwishamalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutua leo Dar esw Salaam.
    Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
    Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
    Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
    Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
    Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
    Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ATUDO AANGUKA MIWILI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top