• HABARI MPYA

    Wednesday, December 12, 2012

    BEKI LA NGUVU LA KENYA LATUA KUSAINI AZAM LEO

    Humphrey Mieno yupo kwenye rada za Azam pia

    Na Mahmoud Zubeiry
    BEKI mmoja matata wa Tusker ya Kenya, anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kwa ajili hya kusaini mkataba wa kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
    Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema jana kwamba, beki huyo mzuri atafichuliwa leo  baada ya kusaini mkataba, ila kwa sasa wanaendelea kuweka kapuni jina lake.
    Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
    Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
    Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
    Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
    Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
    Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BEKI LA NGUVU LA KENYA LATUA KUSAINI AZAM LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top