• HABARI MPYA

    Wednesday, December 12, 2012

    YANGA YAANZA KAZI UHAI CUP LEO


    Na Prince Akbar
    MICHUANO ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom, inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi Kundi C kupigwa.
    Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)
    Timu zinazoshiriki michuano hiyo iliyoanza jana na itamalizika Desemba 23, mwaka huu., zimegawanywa katika makundi matatu, Kundi A likiwa na timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans, Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
    Katika mechi za jana, Azam FC ilianza vema baada ya kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, shukrani kwao, Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo katika mchezo huo wa Kundi B.
    Katika mechi za asubuhi jana, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma na African Lyon iliichapa mabao 4-0 Polisi Moro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA YAANZA KAZI UHAI CUP LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top