Getty Images
KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Cesare
Prandelli amethibitisha kwamba Mario Balotelli, Antonio Cassano na Antonio Di
Natale watakuwamo kwenye kikosi chake cha Euro 2012, lakini amekataa kuwaita
washambuliaji wazoefu, Alessandro Del Piero na Francesco Totti.
Kocha huyo wa timu ya taifa, anatarajiwa
kutaja kikosi chake cha awali cha wachezaji 30 Jumapili, kabla ya kupunguza na
kubaki 23 watakaopanda ndege.
Italia imepangwa kundi moja na mabingwa
watetezi Hispania, Jamhuri ya Ireland na Croatia katika Kundi C kwenye Euro
2012.


.png)
0 comments:
Post a Comment