![]() |
| Niko Christina Mbunda aka Kiroboto |
![]() |
| Mark Zuckieraian kushoto, Dan Kidjo anayemfuatia, Christina Mbunda na Tumaini Meshack wakizungumza na Waandishi leo kuhusu MIN BUZZ mpya |
![]() |
| Shamim Mwasha |
WATAYARISHAJI maarufu wa kipindi cha
runinga cha ‘daladala’ leo wamezindua upya kipindi hiki kwenye televisheni ya
TBC kikiwa na jina jipya la Minibuzz.
Minibuzz ni kipindi kinachoatayarishwa na
MADE IN AFRICA TV, kampuni ya utengenezaji na utayarishaji wa vipindi ambavyo
vina ujumbe kwa ajili ya jamii ya kiafrika..
Awali kilizinduliwa hapa nchini Tanzania
mwaka 2010, kama daladala na kwa muda mfupi sana kilipata wapenzi wengi
takribani watu milioni tatu. Na kwa
mafanikio hayo, kampuni hiyo iliweza kuzindua mfumo huo huo katika nchi ya
Uganda na Kenya.
Mtayarishaji mkuu, Frank Bierens, alisema,
“Jina lipya la Minibuzz linakusudia kuongeza nguvu na kuunganisha Afrika
mashariki. Kwa kufanya kazi chini ya
jina moja na kushirikiana katika utayarishaji, kwa hivyo tunatarajia kuepukana na usumbufu katika soko na kuwa
wazi kwenye makusudio ya kipindi hiki”.
Minibuzz inarekodiwa kila asubuhi ndani ya
gari ndogo aina ya Hiace ambayo ina muundo wa studio. Ina camera, vinasa sauti na vifaa kwa ajili
ya uhariri. Washiriki ni abiria wa
kawaida ambao hupanda basi hili katika vituo mbalimbali nchini kwa ajili ya
kujadili maswala mbalimbali yanayohusu maisha yao.
Kipindi hiki chenye jina jipya kitaendelea
na watangazaji wake Daniel Kijo na Bibi Kiroboto sasa hivi kina sura mpya
kabisa ya Tumaini Meshack.
Watayarishaji wa vipindi wa MADE IN AFRICA
TV –wametangaza uzinduzi wa kipindi cha Radio cha Minibuzz kitacholetwa kwenu
na Bibi Kiroboto akishirikia na Daniel Kijo na Tumaini Meshack. Mfumo huu mpya
unakusudia kuleta mwamko kwa wapenzi na wasikilizaji nchini.
Daniel Kijo amesema, “Nina furaha kubwa kwa
kuzinduliwa kwa kipindi hiki, kama awali hii ni nafasi ya mtu wa kawaida kabisa
kusikika na kuleta changamoto ya mabadiliko Tanzania. Katika mabadiliko ya kipindi hiki,
tunatarajia kuwafikia na kuwaunganisha watanzania wengi zaidi. Kwa kufanya vipindi vya televisheni na
Radio tunaleta muungano katika mipaka yote ya kijamii Tanzania.
Tumaini Meshack ambaye ni mtangazaji mpya
wa kipindi cha Minibuzz amesema, ”Nimefurahi kuungana na timu hii ya Minibuzz
kwani kwa muda mrefu nimekuwa mpenzi wa kipindi hiki. Na sasa, tunatarajia kuungana na watazamaji
wetu wote, katika mada tofauti muhimu za kila siku. Ni kupitia mazungumzo au mijadala, tunaweza
kuendeleza na kuboresha hali ya maisha hapa Tanzania
Akiongezea yaliyosemwa na wenzake, Bibi
Kiroboto naye alikuwa na haya ya kusema, “Mimi nimefurahi zaidi kwa kipindi cha
radio cha Minibuzz kwa vile tutawafikia watanzania wengi zaidi hususani
vijijini. Radio inaikika kila sehemu na wakati wowote.
Kipindi cha Minibuzz cha televisheni
kinarushwa hewani kila siku katika televisheni ya TBC1 saa kumi na mbili
jioni. Kwa redio, ni kila siku saa moja
jioni katika kituo cha radio cha TBCFM.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ms. Eugenia
Chanda kwa simu namba 0713 548496. Au kwa barua pepe, eugeniachanda@yahoo.com





.png)
0 comments:
Post a Comment