![]() |
| Tenga na Robin wakipeana mikono na kubadilishana makabrasha baada ya kusaini mkataba |
| Burudani ya mabinti |
| Tenga na Mgongolwa wakifurahia |
| Tenga na Mgongolwa |
| Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kushoto, katikati mama Juliana Yassoda na kulia Robin |
| Wadau wa soka, Msafiri Mgoyi Mjumbe wa TFF, beki wa zamani Taifa Stars na Meneja wa timu hiyo, Leopold Mukebezi, Fred na kocha Joseph Kanakamfumu |
| Mwandishi wa Nipashe Somoe Ng'itu na kocha Jamhuri Kihwelo |
| Makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mdau Salim |
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), jioni hii
imeingia mkataba wa kuidhamini timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
wa miaka mitano, wenye thamani ya Sh. Bilioni 23.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya
Kempinski, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wakuu wa TFF, TBL na
wadau mbalimbali.
Stars, ambayo tangu mwaka 2006, ilikuwa
ikidhaminiwa na kampuni nyingine ya Bia Tanzania, Serengeti (SBL) sasa itakuwa ikivaa
jezi zenye nembo ya bia ya Kilimanjaro, ambayo pia ni wadhamini wa Simba na
Yanga.
Rais wa TFF, Leodegar Chillah Tenga
alitiliana saini mkataba huo na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche katika
hafla iliyopambwa na burudani nyepesi nyepesi.
Katika hafla hiyo liyofana, utiaji saini wa
mkataba huo, ulishuhudiwa na mawakili wa pande zote mbili, TFF ikiwakilishwa na
Alex Mgongolwa.
Kwa mujibu wa maridhiano hayo, TBL kupitia
bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager itaidhamini Taifa Stars kwa kipindi cha
miaka mitano mfululizo.
Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo
kubwa ya bia kutoa udhamini kwa timu ya taifa, hata hivyo huko nyumba TBL
iliwahi kushiriki katika udhamini wa masuala ya soka kwa miaka minne nyuma huku
ikidhamini Taifa Cup na vilabu vikubwa vya Simba na Yanga.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana
saini, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche alisema udhamini huoi
utafungua mwanga mpya katika medani ya soka nchini Tanzania.
“Tunasaini mkataba wa miaka mitano wenye
thamani ya dola za Marekani milioni 10 na katika kipindi chote hicho kaulimbiu
yetu itakuwa “Fikisha Soka ya Tanzania Katika Kilele cha Mafanikio” na kutupa
kila sababu ya kujivunia kilicho chetu
Tuna matarajio makubwa sana na timu ya
taifa kwani tunaamini kuwa ina uwezo wa kufanya maajabu, na kama nilivyosema
awali, hili ni pambazuko la kuelekea mafanikio. Uwekezaji wetu umelenga katika
kuhakikisha kambi za mazoezi zinaimarishwa, wachezaji watalala katika hoteli
zenye ubora wa juu zenye zaidi ya ngazi tatu zilizo na bwawa la kuogelea na
vifaa vya mazoezi, vifaa vinaboreshwa na pia vijana watapata fursa za kucheza
mechi nyingi za kirafiki ili wajipime nguvu na kupata uzoefu zaidi na timu
zinapata basi jipya la kisasa.
Kwa kuongeza, alisema udhamini wao
utasaidia katikau nunuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa vya michezo, mafunzo
kwa wafanyakazi wa TFF ndani na nje ya nchi, uendeshaji wa tovuti ya TFF, Semina
na mikutano ya utawala bora.
Wakati huo huo, TBL kupitia bidhaa yake
nyingine, Grand Malt, ambacho ni kinywaji kisicho na kilevi itakuwa kikidhamini
Ligi Kuu ya Zanzibar. Hii ni kuonyesha namna TBL ilivyo mstari wa mbele katika
kuhamasisha soka si kwa Bara tu bali na Visiwani. Mkataba huu ni wa miaka
mitatu na utamalizika mwaka 2015 ukiwa na thamani ya Sh milioni 140 kila mwaka.
Kwa upande wake, Rais wa TFF, Lodger Tenga
aliahidi kutoa ushirikiano thabiti kwa wadhamini wapya kwani anaamini mkataba
huo utaleta mapinduzi chanya katika soka nchini Tanzania. Hata hivyo, aliwaomba
Watanzania kuwa na uzalendo kwa timu yao ya taifa kwa kuishangilia kwa wingi
kwenye mechi zake.
“Hakuna
jema lolote kama tutakuwa na ari ya kuzishabikia timu za nje badala ya ya timu
ya nyumbani, wachezaji wetu wanahitaji moyo wawapo uwanjani kwa kushangiliwa ipasavyo,”
alisema.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George
Kavishe alisema udhamini huo ni wa thamani na kwamba watafanya kila
liwezekanalo kuisaidia TFF kuhakikisha kuwa Taifa Stars inang’ara katika anga
za kimataifa na hivyo kukidhi kiu ya Watanzania.
“Hii ni mara ya kwanza kuidhamini Taifa
Stars na tunataka kuja kwa mtindo mpya na wa kipekee, tunataka Watanzania
wajivunie timu yao kwa
sababu ukarimu huanzia nyumbani…tuwape moyo
wachezaji wetu na tujivunie kilicho chetu,” alisema.




.png)
0 comments:
Post a Comment