9 Mei, 2012 - Saa 13:03 GMT
Matatizo Ukraine
Wafuasi wa Tymoshenko
MICHUANO ya Fainali ya Kombe la soka kwa
Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 inayoanza mwezi juni mwaka huu yalikua nuru mpya
kwa taifa la Ukraine kushamiri kwenye medani ya kimataifa na pia kuimarisha
uchumi wake unaolegalega.
Badala yake iliyokua fursa ya kujikwamua
matatizo limekua tatizo.
Katika hatua inayofananishwa na vita
baridi, wakuu wa ngazi ya juu kutoka Muungano wa Ulaya wameapa kua watasusia
mechi zote zitakazopangwa Ukraine kwa sababu ya madai kuhusu kunyanyaswa kwa
Waziri Mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko gerezani.
Wakosoaji wameonya kua mashabiki wa soka
huenda wakashindwa kuhudhuria mechi kutokana na viwango vikubwa vya bei za
kulala hotelini na kwamba serikali ambayo ina upungufu wa fedha imeiweka nchi
hio katika hali mbovu ya uchumi kwa kutumia dola bilioni 14 kuandaa mashindano
haya.
Hi ilikua fursa kwa nchi hii kujiuza na
kuonyesha kiwango chake kwa sababu ya wandishi wa habari watakaokwenda huko kwa
ajili ya mashindano, amesema Oleh Rybachuk, hapo zamani Waziri katika serikali
ya kwanza ya Bi Tymoshenko.
Bw.Oleh ameongezea kusema kua, hivi sasa,
wandishi watakuja kuandika juu ya matatizo mengi kupita kiasi.
Nchi ya Ukrainer ilipewa nafasi ya kuandaa
mashindano ya Euro 2012 kwa ushirikiano na Poland mnamo mwaka 2007 katika hatua
iliyobainika kama zawadi kwa nchi hizi mbili hapo zamani za Kikomunisti
zinazopenda soka.
Wakati huo uchumi wa Ukraine ulikua mzuri
na nchi za magharibi zilifurahia juhudi zake za kukumbatia sera ya demokrasi
kufuatia maandamano makubwa ya mwaka 2004 yaliyojulikana kama ''Orange
Revolution'' yaliyochagiza kuundwa kwa serikali inayopendelewa na Mataifa ya
magharibi.
Ukraine ya leo ni tofauti na ya wakati huo.
Shujaa wa mageuzi yaliyosababishwa na
vuguvugu la Orange, Tymoshenko, wakati huo akiwa kiongozi wa upinzani,
anatumikia kifungo cha miaka saba kwa kutumia vibaya madaraka.
Nchi za magharibi zililalamikia kifungo
chake mwaka jana na kudai kua ni kisingizio cha siasa kilichopangwa na utawala
wa Rais Viktor Yanukovych, ambaye ushindi wake wa mwaka 2004 uliogubikwa na
tuhuma za kuibia kura ulingatuliwa na Bi.Tymoshenko.
Tymoshenko, mwenye umri wa miaka 51, kwa
zaidi ya wiki mbili amesusia chakula baada ya habari kwamba walinzi wa jela
walimfunga ndani ya shuka na kumpiga ngumi za tumbo, huku akilia na kupiga
kelele za kutaka asaidiwe.
Tangu hapo alikua na maumivu makali ya
mgongo.
Picha za majeraha makubwa ya tumbo la
Bi.Tymoshenko na kwenye miguu zilizotolewa na shirika maarufu nchini humo la
haki za binadamu, zimeushangaza ulimwengu na kua sababu ya Maofisa wa Muungano
wa Ulaya, akiwemo Rais wa Muungano Herman Van Rompuy, vilevile Rais wa tume ya
Ulaya Jose Manuel Barroso, halikadhalika serikali za Austria na Ubeligiji
zimesimamisha mipango ya kuhudhuria mechi zitakazochezwa huko Ukraine.
Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani
amedokeza kua ataweza kuzuru nchi hio wakati wa amshindano ikiwa serikali
itabadili jinsi inavyomtunza Bi.Tymoshenko.
Katika tukio la aibu zaidi kwa nchi hio,
imebidi mipango ya kikao juu ya ushirikiano wa Mataifa ya Ulaya ya kati na
mashariki kwa sababu viongozi wengi walisusia kutokana na suala la kuteswa kwa
Tymoshenko.
Ikiwa hayo hayatoshi kuichafulia jina
Ukraine, Mkuu wa UEFA, Michel Platini amelalamika juu ya viwango vya bei ya
hoteli na kuitaka serikali isiwaruhusu majambazi kuwapora wapenzi wa soka.
Katika vichekesho vingine, tangazo la TV
huko Uholanzi limezua kasheshe kuhusu mashindano ya EURO 2012.
Kampuni ya umeme ya Uholanzi katika tangazo
la biashara lililotolewa hivi karibuni inawashauri wanawake wasiwaruhusu waume
wao kuhudhuria mechi za Ukraine kwa sababu hawawezi kuponyoka urembo wa
wanawake wa Ukraine. Ukraine imelalamika na kusema tangazo hilo ni la
kiubaguzi.


.png)
0 comments:
Post a Comment