9 Mei, 2012 - Saa 14:52 GMT
Usain Bolt
David Rudisha
BINGWA wa dunia wa mbio za mita 800 ikiwa
anatazamiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mjini
London, David Rudisha, anasema ana tamaa ya kupambana na Usain Bolt katika mbio
zinaostahili wote wawili.
Akizungumza mbele ya wandishiwa habari
kabla ya mashindano ya Diamond League mjini Doha yatakayofanyika siku ya
Ijumaa, Rudisha amesema ametafakari uwezekano wa kushindana na Bolt kwa mbio
ambazo angeanza kwa kujiandaa ingawa haoni hilo likitimia.
Mkenya huyo alichagua mbio za mita 400 kupokezana
vijiti kama mbio za kutimiza ndoto yake, ambapo wangechuana katika mbio ambazo
wote wanazipenda.
Rudisha amesema kua ingembidi yeye ashuke
kutoka mbio za mita 800 huku Bolt akipanda kutoka mbio zake za mita 100 na 200
kusawazisha uwezo wa kila mmoja.
Rudisha, hukimbia mbio za mita 400
kuzidisha kasi yake na amesema huko Doha kua Usain Bolt ana kasi, mimi sina
kasi kama yake lakini nina kasi inayoniwezesha kwenda mwezo mrefu. Ndiyo sababu
ingefurahisha kuona jinsi mwisho ungekuaje.
Rudisha, anashiriki mbio za Doha bila
jeraha na anasema kua mbio hizi zitamsaidia kujinoa kwa ajili ya mashindano ya
mjini London.
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23
amefanikiwa katika mbio hizi ingawa bado hajafanikiwa kushinda medali ya
dhahabu, ameongezea kusema kua akiweza kuweka mda bora mjini Doha basi atajiona
kua tayari na njiani kufanikisha ndoto ya kujishindia medali ya dhahabu.
Mjini Doha, hatokua na mpinzani mkali baada
ya Mohammed Aman kujiondoa kwenye mashindano.
Kijana huyo kutoka Ethiopia mwenye umri wa
miaka 18 alimshinda Rudisha kwenye mbio za mjini Milan mwezi Septemba mwaka
jana mjini Milan na pia kwenye mashindano ya Dunia mnamo mwezi March mwaka huu.


.png)
0 comments:
Post a Comment