Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya

HAZARD AZIWEKA NJIA PANDA MAN CITY, CHELSEA

MSHAMBULIAJI wa Lille ya Ufaransa, Eden Hazard mwenye umri wa miaka 21, amefunguka kuhusu nia na dhamira yake ya kuhamishia cheche zake katika Ligi Kuu ya England, akisema anatamani kuvaa jezi za rangi ya bluu, maana yake anaweza akatua Manchester City au Chelsea, ambazo zote zimgombea.
KIMENUKA. ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa, baada ya beki la nguvu la kati la Ajax Amsterdam ya Uholanzi, Jan Vertonghen kuionya klabu yake isithubutu kumuuza kwenda klabu ya Tottenham ya England.
Yann M'Vila
M'Vila amecheza mechi 36 za Ligue 1 msimu huu.
KLABU ya Arsenal imekubali kutoa dau la pauni Milioni 17 kwa klabu ya Rennes ya Ufaransa, ili kumnasa mchezaji mwenye umri wa miaka 21, Yann M'Vila. Dili hiyo inatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa wiki.
WASHIKA Bunduki wa London, wataendelea na mpango wao wa kumsajili kipa wa Swansea, Michel Vorm.
KLABU ya Liverpool inajipanga kufufua mpango wake wa kumsajili Mholanzi, Eljero Elia, ambaye walimtaka awali alipokuwa Hamburg. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameshindwa kuwika akiwa Juventus ya Italia na yuko tayari kuondoka nchini humo, kutafuta timu ambayo atakuwa na namba kwenye kikosi cha kwanza.
BEKI wa kushoto wa klabu ya Everton, Leighton Baines mwenye umri wa miaka 27 amegeuka lulu na atahitaji utulivu kuchukua uamuazi sahihi aende klabu gani kati ya Manchester United ya England pia na Bayern Munich ya Ujerumani, ambazo zote zinamtaka.
KOCHA wa Aston Villa, Alex McLeish amemtambulisha kiungo mwenye umri wa miaka 29 wa Wolves, Karl Henry kama mtu atakayejiunga na klabu yake mwishoni mwa msimu, kuongeza nguvu kutokana na uzoefu wake.

TERRY KUTEMWA ENGLAND

BEKI wa Chelsea, John Terry anaweza kupigwa chini kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, chini ya kocha Roy Hodgson kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.
KLABU ya West Brom iko kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Chelsea na Inter Milan, Claudio Ranieri achukue nafasi ya kocha wao, Roy Hodgson aliyechukuliwa na timu ya taifa ya England.
KOCHA wa muda wa Wolves, Terry Connor anaweza kupewa mkataba wa kudumu wa ajira, baada ya kufanyiwa usaili katika kuwaniwa nafasi hiyo.

MOURINHO AIFUATILIA CHELSEA:

KIUNGO wa Real Madrid, Xabi Alonso, ambaye aliichezea misimu mitano Liverpool kabla ya kutimkia Bernabeu, aliwekwa benchi na kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho, aliyewahi kuifundisha  Chelsea ili afuatilie matokeo ya timu zao hizo za zamani katika fainali ya Kombe la FA Jumamosi, ingawa siku hikyo Real walikuwa wana mechi ya ugenini ya ligi dhidi ya Malaga. Alonso alikuwa benchi akifuatilia matokeo ya mechi hiyo kwa simu yake ili amuambie Mourinho.
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba ametoa bonge la mshangao kwa watu, baada ya kutokea kwenye video ya muziki ya mwimbaji wa KIfaransa, Julia Channel
.