BEKI wa kimataifa wa Hispania, anayechezea klabu ya Barcelona, Carles Puyol anaweza kuzikosa Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 baada ya kuumia na kutakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34, alikaa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu, mapema mwaka huu kwa maumivu ya goti na Barca imethibitisha sasa anatarajiwa kuwa nje kwa wiki sita.
"Baada ya kufanyiwa vipimo, imeamualiwa atafanyiwa upasuaji Mei 12," ilisema klabu hiyo.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Hispania kitacheza mechi ya kwanza ya Euro 2012 dhidi ya Italia Juni 10.
Kocha wa Hispania, Vicente Del Bosque, anatarajiwa kutaja kikosi chake cha kwanza Mei 15, mwaka huu kabla ya kupunguza wachezaji na kubakiza idadi ya kwenda nao kwenye michuano hiyo Mei 27, mwaka huu.
Beki mzoefu, Puyol alitonesha goti lake Jumamosi katika mechi dhidi ya Espanyol, Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.

MATAJI YA PUYOL:
TIMU YA TAIFA
Kombe la Dunia 2010
Euro 2008
KLABU:
Barcelona La Liga: 2004-2005, 2005-2006, 2008-2009, 2009-2010, 2010-2011
Ligi ya Mabingwa: 2005-2006, 2008-2009, 2010-2011
Uefa Super Cup: 2009, 2011
Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2009, 2011
Kombe la Mfalme: 2008-200
9