Di Matteo
AdChoices |
NAHODHA wa Chelsea, John Terry anaamini ushindi wa Kombe la FA utamuwezesha Kocha wa Muda, Roberto Di Matteo kupewa ukocha wa kudumu katika klabu hiyo.
Di Matteo ameonekana mwenye mafanikio tangu aichukue Chelsea, akirithi mikoba ya aliyekuwa bosi wake, Andre Villas-Boas aliyefukuzwa Machi, mwaka huu baada ya kufikisha klabu katika fainali mbili, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa.
Pamoja na hayo, bado Chelsea inasota kuhakikisha inamaliza ndani ya nne bora kwenye Ligi Kuu, ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao na Terry amemwagia sifaDi Matteo kwamba amefanya mambo makubwa katika kipindi kifupi.
Mustakabali wa Di Matteo Stamford Bridge bado haujulikani na Chelsea imesistiza hakuna uamuzi utakaochukuliwa kuhusu mrithi wa Villas-Boas hadi msimu uishe.
Pamoja na hayo, Terry amewaambia Waandishi wa Habari jana kwamba ushindi dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Wembley leo utainenepesha CV ya Di Matteo.
0 comments:
Post a Comment