Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

JUVENTUS YAMTAKA VAN PERSIE

KIBIBI kizee cha Turin, Juventus imekuwa klabu ya kwanza kuelezea waziwazi nia yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Robin Van Persie, lakini Arsenal wanajiamini watambakiza mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Uholanzi Uwanja wa Emirates.
KLABU ya Manchester United imeonyesha nia ya dhati kabisa ya kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 28, Van Persie, ambaye amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa na klabu yake, Arsenalt, na kocha Sir Alex Ferguson amepania kupambana kwa jeuri ya fedha na mahasimu wake wa jadi, Manchester City sokoni kumnasa mshambuliaji huyo.
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson pia anajiandaa kukata dau la pauni Milioni 10 kuinasa saini ya beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines.
KLABU ya Chelsea imengia katika mtego wa kuwaboa mashabiki wake kwa kumuachia mshambuliaji wake, Didier Drogba aondoke mwezi huu - baada ya ombi la Nahodha huyo wa Ivory Coast kutaka mkataba mpya wa miaka miwili kukwama.
Everton defender Leighton Baines
Leighton Baines has scored 11 Premier League goals since moving to Everton in 2007
KLABU ya Liverpool ya England imeingia kwenye harakati za kuwania saini ya winga wa Juventus ya Italia, mwenye umri wa miaka 27, Mserbia Milos Krasic. 
KOCHA wa Wekundu wa Anfield, Kenny Dalglish pia anamtolea jicho mchezaji wa Real Madrid, Hamit Altintop, mwenye umri wa miaka, kama mbadala wa Dirk Kuyt, ambaye anatakiwa na Hamburg.

SHEIKH MANSOUR AJITOA MAN CITY V QPR...

MMILIKI wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansour hatarajiwi kuwa katika Uwanja wa Etihad Jumapili kushuhudia timu yake hiyo, Manchester City ikimenyana na Queens Park Rangers mechi ambayo wakishinda wanakuwa mabingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 44. Amesema anapenda kuiangalia mechi hiyo kupitia televisheni.
KOCHA Gus Poyet yuko mbioni kuachia ngazi katika klabu ya Brighton, baada ya klabu tatu za West Midlands kuonyesha nia ya kumchukua. West Brom na Wolves iliyoshuka daraja zinasaka kocha mpya na Aston Villa inajifikiria upya kuendelea na Alex McLeish baada ya kuwaangusha katika msimu wake wa kwanza kazini.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Andy Carroll anatumai amesuuza nafsi ya kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson baada ya kufunga mabao mfululizo katika mechi za mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya England. Carroll amefunga mabao tisa msimu huu, matatu katika mechi sita zilizopita.
MSHAMBULIAJI wa West Brom, Shane Long amesema kwamba The Baggies inahitaji "kocha mkubwa" kuchukua nafasi ya Hodgson, aliyehamia timu ya taifa ya England, ambaye aliifundisha kwa mara ya mwisho timu hiyo Jumapili kabla ya kwenda kuanza maandalizi ya Euro 2012.
Manchester City owner Sheikh Mansour
Sheikh Mansour completed his purchase of Manchester City in 2008
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa England, chapombe Paul Gascoigne 'Gazza' ana wasiwasi Newcastle itapoteza wachezaji wake fulani muhimu watakaohamia klabu kubwa Ulaya mwishoni mwa msimu- hata kama kikosi hicho cha Alan Pardew kitakata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
WACHEZAJI wawili wa Newcastle, Hatem Ben Arfa na Yohan Cabaye ni miongoni mwa wachezaji nane, ambao wataivaa England, baada ya kutajwa kwenye kikosi cha Ufaransa cha Euro 2012 kitakachoingia kambini.
FMCHEZAJI wa zamani wa Everton, Ian Snodin amesema kumsajili Steven Pienaar, ambaye anacheza kwa mkopo kutoka Tottenham, lazima kiwe kipaumbele cha kocha David Moyes katika dirisha la usajili.

BALOTELI AMTIBUA MANCINI...

MSHAMBULIAJI mtata, Mario Balotelli alitulizwa kwenye mazoezi ya timu yake Manchester City jana, baada ya kumtibua kocha wake Roberto Mancini, ambaye alimnyooshea kidole kwa hasira, wakati wakijiandaa na mechi dhidi ya QPR kukamilisha ligi. Sasa Balotelli yuko kwenye hatari ya kuwekwa benchi kwenye mechi na QPR.
listen here: Mario Balotelli was taken to one side to be spoken to by manager Roberto Mancini
Mario Balotelli akizinguana na kocha Roberto Mancini
listen here: Mario Balotelli was taken to one side to be spoken to by manager Roberto Mancini
 Mancini akimuadabisha Balo
Back with the boys: After his talking to, Balotelli joined in with the rest of the title-chasing squad
Balotelli na wenzake mazoezini