Quinton Fortune enzi zake Manchester United
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester
United, Quinton Fortune amesema yuko tayari kuifundisha timu ya Taifa ya Vijana
ya Tanzania chini ya miaka 17 kama atapewa nafasi hiyo kwa sababu kiu yake ni
kuona soka ya Kusini mwa jangwa la Sahara inakuwa na kufikia kiwango cha Afrika
Magharibi na Kaskazini.
Gazeti la Mwananchi leo, kwamba; walizungumaza
Na mchezaji huyo jana mjini Dar es Salaam, akasema
ingawa haifahamu rekodi ya timu ya Taifa ya Tanzania, lakini anaamini kama
atapata nafasi ya kuifundisha timu ya vijana itakuwa ni faraja zaidi kwani
atakuwa ametimiza kiu yake ya kufundisha soka na kuinua kiwango cha soka la
Afrika ya Mashariki.
Fortune ambaye yuko nchini kwa lengo la
kuzindua mashindano ya vijana ya Airtel Raising Stars, alisema anaamini
wachezaji wa Ukanda huu wa Sahara wana matatizo yanayofanana na ndiyo sababu ya
kushindwa kucheza soka katika ligi kubwa duniani kama England.
"Matatizo ya vijana wengi ni elimu ya
soka, wana vipaji, lakini lazima upate elimu kwanza ili uweze kufanya vizuri
katika soka,"alisema Fortune.
Fortune alisema tatizo lingine ni kushindwa
kutafsiri mikataba mbalimbali ya soka, kushindwa kutambua umuhimu na malengo
yao katika soka la kimataifa.
Alisema yeye alifanikiwa kucheza Ulaya kwa
sababu aliondoka kwao akiwa na miaka 14 na kujiunga na klabu za huko ambazo
zilimtunza kufikia hapo.
"Baada ya kumaliza kozi yangu ya
ukocha pamoja na kumaliza kazi nilizopewa na klabu yangu ya Manchester United
nitarudi Tanzania rasmi kwa ajili ya kufuatilia soka la Tanzania kwa undani
zaidi pamoja na kutafuta vipaji na kufuatilia zoezi la Airtel Rasing Stars
linavyoendelea pamoja na kuangalia maendeleo yao baada ya hapa,"alisema
Fortune.
Mbali na Uzinduzi huo pia Fortune
alitembelea Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongolamboto na kucheza soka na
wanafunzi wa shule hiyo huku akikabidhi madawati 30 mipira 40 na jezi jozi
tatu.
0 comments:
Post a Comment