Drenthe kushoto akizinguana na Messi
WINGA wa Everton, Royston Drenthe amemshushia
shutuma nzito, Mwanasoka Bora wa Dunia mara tatu, Lionel Messi, akidai kwamba
nyota huyo wa Barcelona alimuita 'negro' (mtu mweusi) zaidi ya mara moja
uwanjani.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi,
alikutana uwanjani mara kadhaa na Muargentina huyo wakati akichezea Real Madrid
na Hercules, na amesema wakati wote alikuwa anakwaruzana na Messi akiwa hana
mpira.
"Tumecheza sana tu dhidi yake, na wakati
wote tulikuwa tunazinguana. Unajua nini kinachonisumbua sana mimi? Ile sauti
ambayo ainiita 'negro, negro'," Drenthe alisema kwenye mahojiano na jarida
la Helden la Uholanzi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Drenthe
kwa sasa anachezea Everton ya Ligi Kuu England kwa mkopo na anapenda kuhamia
moja kwa moja katika klabu hiyo.


.png)
0 comments:
Post a Comment