MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Mbwana
Ally Samatta ‘Sama Goal’ ameendeleza makali yake ya kufunga mabao katika klabu
yake ya Tout Puissant Mazembe, baada ya jana kuichapa mabao 6-0 Elima katika
Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Frederic Kibassa Maliba, Lubumbashi, mshambuliaji mpya wa Mazembe, Hope
Traore kutoka Mali alifunga mabao matatu peke yake, akiichezea mechi ya kwanza
klabu hiyo.
Mbali na bao la Samatta, mabao mengine ya
Mazembe yalitupiwa kimiani na Kanda Lungu na Sinkala Tusilu.
TPM sasa inaongoza ligi kwa wastani wa
pointi mbili dhidi ya Vita Club inayoshika nafasi ya pili, 19-17.
Mazembe wanatarajiwa kuondoka kesho kwenda
Khartoum, Sudan tayari kwa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi
ya El Merreikh kwenye Uwanja wa Omduran.
Mazembe ilishinda 2-0 mechi ya kwanza na
huko inahitaji sare ili kusonga mbele.
Ikiwa huko, Samatta na mchezaji mwenzake wa
zamani wa Simba, Patrick Ochan, watakutana na timu yao hiyo ya zamani, ambayo
mwishoni mwa wiki hii inacheza na Al Ahly Shandy katika mchezo wa marudiano wa
Kombe la Shirikisho.



.png)
0 comments:
Post a Comment