• HABARI MPYA

    Monday, May 07, 2012

    VIPIGO VYA MBWA MWIZI SIMBA ILIVYOWAHI KUIPA YANGA


    Okwi leo alikaribia kuvunja rekodi ya hat-trick yas Kibadeni ya 1977. Wengi wanajiuliza penalti ya Mafisango kwa nini asipewe yeye akamaliza kazi?

    LIGI KUU
    JULAI 19, 1977
    Simba v Yanga
    6-0
    WAFUNGAJI:
    Abdallah Kibadeni dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20.

    JULAI 2, 1994
    Simba v Yanga
    4-1
    WAFUNGAJI:
    Simba: George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani, Dua Saidi Yanga; Constantine Kimanda.

    MEI 6, 2012
    Simba v Yanga 5-0
    WAFUNGAJI: Emmanuel Okwi dak 1 na 52, Felix Sunzu dk47, Juma Kaseja dk 66 na Patrick Mafisango dk 73.

    KOMBE LA TUSKER:
    MACHI 31, 2002.
    Simba Vs Yanga 4-1
    WAFUNGAJI:
    SIMBA: Mark Sirengo dk. 3 na 76, Madaraka Selemani dk. 32 na Emanuel Gabriel dk. 83.
    YANGA: Sekilojo Chambua dk 16.
    (Mechi hii ya fainali iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, FAT).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIPIGO VYA MBWA MWIZI SIMBA ILIVYOWAHI KUIPA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top