![]() |
| Kaseja |
JUMA Kaseja, kipa wa SImba SC leo amevunja
rekodi ya kipa wa zamani wa timu hiyo, Iddi Pazi ‘Father’ ya kufunga bao dhidi
ya watani wa jadi, Yanga.
Pazi alifunga kwa penalti mwaka 1984 katika
sare ya 1-1 na Yanga, wakati leo Kaseja amefunga bao la nne, Simba ikiifunga
Yanga 5-0 Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Mwameja Mohamed ni kipa mwingine
aliyewafunga Yanga kwa penalti, lakini yeye alifunga baada ya dakika 120 za
sare.
Kaseja anaelekea kuweka rekodi ya kuwa kipa
bora wa kihistoria kuwahi kutokea SImba, kwani akiwa katika mwaka wake wa tisa
tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2003 bado yuko juu na bado anaibeba timu.
Japokuwa Simba wamepita makipa wengi bora, wakiwemo
Omar Mahadhi ‘Bin Jabir’, Athumani Mambosasa (wote marehemu) na Iddi Pazi,
lakini kwa sasa Mwameja ndiye aliyeiletea mafanikio makubwa zaidi timu hiyo,
akiifikisha fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 na kuipa mataji manne ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, 1992, 1995, 1996 na 2002.



.png)
0 comments:
Post a Comment