![]() |
Kiiza wa Yanga kushotona Chollo wa Simba kulia |
KIINGILIO cha chini katika mechi ya wapinzani wa jadi, Simba na Yanga keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa Sh. 5,000 na kwa vibosile wa ukweli, yaani VIP A itakuwa ni Sh. 30,000- huko unashuhudia mechi kwa raha zote.
WAKATI vinara wa ligi kuu bara Simba
wakitarajiwa kutua jijini leo tayari kwa mchezo wao dhidi ya mahasimu wao Yanga
kesho kwenye dimba la Taifa, mahasimu wao Yanga wameficha juu ya ujio wao.
Timu hizo zinatarajiwa kukwaana kwenye
dimba la taifa katika moja ya mchezo wa funga dimba la ligi hiyo itakayofikia
tamati hiyo kesho.
Akizungumza na gazeti hili jana,ofisa
habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kitatua leo
kwa ndege maalum kutoka Visiwani Zanzibar kilipokwenda kujiandaa na mchezo huo.
Alisema wachezaji wote wapo katika hali
nzuri na wameapa kucheza kufa kupona kuhakikisha wanashinda mchezo huo ambao
kama mambo yakienda vema watatangaza ubingwa wa msimu wa 2011/2012.
“Kikosi chetu chote kipo fiti na vijan a
watakuja kesho (leo)kwa ndege maalum na kisha wataelekea katika hoteli moja ya
kitalii kwa ajili ya kusubiria mchezo wetu na Yanga,”alisema.
Kwa upande wa Yanga kupitia kwa msemaji wao
Louis Sendeu, kikosi cha timu hiyo kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kipo katika
hali nzuri wakiendfelea na maandalizi ya
mchezo huo, huku viongozi wakiwajenga zaidi kisaikolojia.
Hata hivyo Sendeu alishindwa kuweka wazi ni
lini timu yao itarejea jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Bagamoyo na Dar es
Salaam hakuna umbali mkubwa hivyo timu itarejea siku yoyote.
Katika hatua nyingine, kiingilio cha chini
katika mchezo huo kinatarajiwa kuwa sh.5,000 kwa watakaokaa jukwaa la kijani
bluu, wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi 40,000 kitakachohusisha
mashabiki watakaokaa jukwaa la VIP A.
Mashabiki watakaokaa VIPB watalipa
sh.30,000, VIP B shilingi 20,000 huku watakaokaa jukwaa la orange watalipa
shilingi 10,000.
0 comments:
Post a Comment