• HABARI MPYA

    Wednesday, April 16, 2025

    YANGA NA JKT TANGA, SIMBA NA SINGIDA MANYARA MEI 16


    MABINGWA watetezi, Yanga SC watasafiri hadi Tanga kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya JKT Tanzania kati ya Mei 16 na Mei 18 Uwanja wa Mkwakwani.
    Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo iliyo katika mwaka wa pili wa udhamini wa Benki ya CRDB itazikutanisha Simba na Singida Black Stars Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Yanga walitinga Nusu Fainali kwa ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Stand United jana Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Kwa upande wao JKT Tanzania iliitoa Pamba Jiji FC ya Mwanza juzi kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
    Simba SC  ilifungua milango ya Nusu Fainali kwa kuitupa nje Mbeya City kwa kuichapa mabao 3-1  Jumapili Uwanja wa KMC na Singida Black Stars iliitoa Kagera Sugar kwa kuifunga mabao 2-0 Uwanja wa CCM LITI mjini Singida juzi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA JKT TANGA, SIMBA NA SINGIDA MANYARA MEI 16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top