• HABARI MPYA

    Sunday, April 20, 2025

    SIMBA SC YAICHAPA STELLENBOSCH 1-0 ZANZIBAR BAO LA AHOUA


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza was Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45'+2 kwa shuti la kitaalam la mpira wa adhabu lililomshinda kipa wa Afrika Kusini, Oscarine Masuluke.
    Timu hizo zitarudiana Aprili 27 kuanzia Saa 10:00 jioni pia Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban, Afrika Kusini na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla Kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria katika Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA STELLENBOSCH 1-0 ZANZIBAR BAO LA AHOUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top