• HABARI MPYA

    Sunday, April 27, 2025

    TANZANIA YAINGIA NUSU FAINALI MICHUANO YA FUTSAL AFRIKA WANAWAKE


    TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Michuano ya Futsal Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal kwenye mchezo wa mwisho wa KUndi C jana Uwanja wa Salle Moulay Abdellah Jijini Rabat nchini Morocco inakofanyika michuano hiyo.
    Mabao ya Tanzania yalifungwa na Donisia Minja dakika ya 13, Vaileth Nicholas Mwamakamba dakika ya 20 na Anna Katunzi dakika ya 21, wakati la Senegal lilifungwa na Ndeye Kane dakika ya 29 - na sasa itamenyana na Morocco kesho kuanzia Saa 2:00 usiku hapo hapo Salle Moulay Abdellah Jijini Rabat.
    Kipa wa Tanzania na klabu ya JKT Queens, Najiat Abbas Idrisa alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi hiyo baada ya kazi nzuri ya kuzuia michomo ya wapinzani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAINGIA NUSU FAINALI MICHUANO YA FUTSAL AFRIKA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top