• HABARI MPYA

    Tuesday, January 07, 2014

    SIJAONA BEKI KAMA WILLY MARTIN ‘GARI KUBWA’, ASEMA PROMOTA WAKUGANDA

    Na Princess Asia, Zanzibar
    PROMOTA maarufu wa soka nchini, George Wakuganda amesema kwamba bado hajaona beki bora wa kati kama alivyokuwa Willy Martin ‘Gari Kubwa’ aliyewika Ushirika ya Moshi, Yanga, Simba SC za Dar es Salaam na Majimaji ya Songea.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa, Wakuganda ambaye huandaa mechi za kimataifa nchini, amesema kwamba Gari Kubwa enzi zake alikuwa beki mwenye nguvu na pumzi, ambaye aliwadhibiti washambuliaji wengi hatari.
    “Kwa kweli siku hizi wanakuja mabeki wanasifiwa sana, ila mimi kwangu mwanaume yule tangu aondoke uwanjani, sijaona mwingine kama yeye. Alikuwa beki, beki kweli,”alisema Wakuganda.    
    Gari Kubwa; Hivi karibuni Willy Martin alitokea kwenye mazoezi ya Simba SC Uwanja wa Kinesi

    Wakuganda alikuwa Zanzibar kushuhudia michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo inatarajiwa kufikia tamati Januari 13, tangu ianze Januari 1, mwaka huu.
    Willy Martin ‘Gari Kubwa’ alisajiliwa Yanga SC mwaka 1993 akitokea Ushirika ya Moshi mkoani Kilimanjaro hadi 1995 alipotemwa akaenda Majimaji ya Songea kabla ya kusajiliwa Simba SC mwaka 2000, alikocheza hadi kwa misimu miwili na kustaafu.
    Willy Martin 'Gari Kubwa' wa kwanza kushoto waliochuchumaa katika kikosi cha Yanga SC 1994

    Gari Kubwa pia aliwahi kuwa Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars enzi zake.  John Jacob Mwansasu ‘Sol Campbell’ ni kizazi kilichofuatia cha mabeki wazuri baada ya akina Willy Martin ‘Gari Kubwa’, ambaye naye pia aliwika Yanga na Taifa Stars.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIJAONA BEKI KAMA WILLY MARTIN ‘GARI KUBWA’, ASEMA PROMOTA WAKUGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top