TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya Futsal Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cameroon leo Uwanja wa Salle Moulay Abdellah Jijini Rabat nchini Morocco inakofanyika michuano hiyo.
Mabao ya Tanzania yamefungwa na Vaileth Nicholas dakika ya 31, Aisha Mnunka dakika ya 35 na Anastazia Katunzi dakika ya 38, wakati ya Cameroon yamefungwa na Pekure dakika ya 32 na Beulou dakika ya 36.
Tanzania sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Morocco na Angola wanaomenyana muda huu hapo hapo Uwanja wa Salle Moulay Abdellah.
Nahodha wa Tanzania, Vaileth Nicholas Mwamakamba ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mchezo huo.
Aisha, kwa kuingia Fainali Tanzania imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia la Futsal zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Ufilipino kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 7.
0 comments:
Post a Comment