• HABARI MPYA

    Wednesday, April 30, 2025

    TANZANIA YAANZA VIBAYA AFCON U20, YACHAPWA 1-0 NA AMAJITA


    TANZANIA imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika  kwa vijana chini ya Umri wa miaka 20 baada ya kuchapwa bao 1–0 na Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa  Suez Canal Jijini Ismailia nchini Misri inakofanyika michuano hiyo.
    Bao pekee la Amajita lililoizamisha Ngorongoro Heroes limefungwa na Shakeel April wa Cape Town City dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya Mogamat Faiz Abrahams wa Stellenbosch, wote viungo.
    Ngorongoro Heroes itashuka tena dimbani Mei 3 kumenyana na  Sierra Leone, kabla ya kucheza na Zambia Mei 6 na kukamilisha mechi zake za Kundi A Mei 9 kwa kumenyana na wenyeji, Misri. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAANZA VIBAYA AFCON U20, YACHAPWA 1-0 NA AMAJITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top