• HABARI MPYA

    Sunday, April 27, 2025

    SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


    TIMU ya Simba imefanikiiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Stellenbosch katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali jioni ya leo Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban, Afrika Kusini
    Simba wananufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Jumapili iliyopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, bao pekee la kiungo wa Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45'+2.
    Simba sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria ambazo zinarudiana leo kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine.
    Ikumbukwe RSB Berkane ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90'+2 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top