• HABARI MPYA

    Sunday, April 20, 2025

    NAMUNGO FC YAICHAPA MASHUJAA 2-1 RUANGWA


    WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
    Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Derick Mukombozi dakika ya 28 na Erasto Nyoni dakika ya 87, wakati bao pekee la a Mashujaa limefungwa  na Jaffar Kibaya kwa penalti dakika ya 25.
    Kwa ushindi huo, Namungo FC wanafikisha pointi 31 katika mchezo wa 27 na kusogea nafasi ya nane, wakiishushia nafasi ya tisa Mashujaa inayobaki na pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA MASHUJAA 2-1 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top