• HABARI MPYA

    Sunday, April 27, 2025

    BARCA WAICHAPA REAL MADRID 3-2 NA KUTWAA KOMBE LA MFALME HISPANIA


    TIMU ya FC Barcelona jana ilifanikiwa kutwaa Kombe la Mfalme Hispania baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid Uwanja wa Olímpico de Sevilla Jijini Sevilla.
    Pedri alianza kuifungia Barca dakika ya 28, kabla ya Real kutoka nyuma na kuongoza kwa mabao ya Wafaransa, mshambuliaji Kylian Mbappé dakika ya 70 na kiungo Aurélien DjaniTchouaméni dakika ya 77.
    Mshambuliaji Ferran Torres akaisawazishia Barca dakika ya 84 na mchezo ukahamia kwenye dakia 30 za nyongeza – ndipo mshambuliaji Mfaransa mwenye asili ya Benin, Jules Olivier Koundé alipoifungia Barcelona bao la ushindi dakika ya 116.
    Wachezaji watatu wa Real Madrid, walitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia fujo refa, Ricardo De Burgos kufuatia Barca kupata bao la ushindi - wawili waliokuwa benchi tayari baada ya kufanyiwa mabadiliko, Antonio Rudiger na Lucas Vázquez pamoja na Jude Bellingham aliyekuwa uwanjani bado, ambaye alionyeshwa kadi ya pili ya njano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA WAICHAPA REAL MADRID 3-2 NA KUTWAA KOMBE LA MFALME HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top