• HABARI MPYA

    Sunday, April 27, 2025

    NI RSB BERKANE NA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO


    TIMU ya RSB Berkane ya Morocco na itakutana na Simba katika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa CS Constantine leo nchini Algeria licha ya kufungwa bao 1-0.
    Katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine — bao pekee la CS Constantine lilifungwa na mshambuliaji Abdennour Iheb Belhocini dakika ya 47, lakini RSB Berkane wanafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kushinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.  
    Mabao ya RSB Berkane siku hiyo yalifungwa na mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90'+2.
    Berkane itakutana na Simba ambayo imeitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini jioni ya leo kufuatia sare ya bila mabao katika mchezo mwingine wa marudiano wa Nusu Fainali Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban.
    Simba nayo imenufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita pia Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, bao pekee la kiungo wa Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45'+2.
    Berkane itaanzia nyumbani katika mchezo wa kwanza wa Fainali Mei 17, kabla ya timu hizo kurudiana Mei 25 Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI RSB BERKANE NA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top