WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na kiungo Bakari Msimu dakika ya 27 na mshambuliaji kutoka Mali, Amara Bagayoko dakika ya 37, wakati bao pekee la Ken Gold limefungwa na mshambuliaji Sadallah Lipangile dakika ya 39.
Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya nane, wakati Ken Gold wanabaki na pointi zao 16 wakiendelea kushika mkia baada ya timu zote kucheza mechi 27.
Aidha, matokeo hayo yanamaanisha rasmi Ken Gold iliyopanda Ligi Kuu msimu kama mabingwa wa Championship wamekwishashuka daraja, kwani hata kama watashinda mechi zao tatu za mwisho watamaliza na pointi 25 ambazo zimekwishavukwa na Tanzania Prisons yenye pointi 27.
Ligi Kuu inashirikisha timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

0 comments:
Post a Comment