AFISA habari wa Yanga, Ally Shaaban Kamwe ametozwa Faini ya Sh. Milioni 5 na kupewa onyo la kutorudia kosa la Kimaadili ndani ya miaka miwili kuanzia Aprili 16, mwaka huu (2025).
Naye Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally hajakutwa na hatia juu ya makaosa ya Kimaadili yaliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Maadilia ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kukosekana ushahidi wa kutosha.
Viongozi kadhaa wamechukuliwa hatua todauti kwa makosa ya Kimaadili yaliyowasilishwa mbele ya Kamati hiyo, pigo kubwa likienda kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Temeke (TEFA), Salehe Mohamed Salehe na waliokuwa Makamu Mwenyekiti Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shufaa Jumanne Nyamlani ambao wamefungiwa maisha kujihusisha na Soka.
0 comments:
Post a Comment