• HABARI MPYA

    Saturday, May 12, 2012

    TAIFA QUEENS YANG'ARA NETIBOLI AFRIKA


    GS wa Taifa Queens akipiga mishe kwenye lango la Botswana

    TIMU ya taifa ya Netiboli ya Tanzania, Taifa Queens imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Afrika ya Netiboli, yaliyofikia tamati leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kuifunga Botswana 32-23 usiku huu.
    Malawi imeteta ubingwa wake- wakati Zambia imekuwa ya tatu katika michuano hiyo iliyoshirikisha nchi sita, nyingine zikiwa ni Botswana, Zambia na Lesotho.
    Mechi hiyo iliyokuwa ianze saa 7:30 mchana, Uwanja wa Taifa wa nje, ilichelewa kuanza kutokana na mvua kali, hivyo kuhamishiwa Uwanja wa ndani.
    Hata hivyo, Uwanja wa ndani nako kukawa hakuna umeme, hivyo zikafanyika jitihada za kuwasiliana na TANESCO warejeshe umeme eneo hilo, ambazo zilizaa matunda sa 12 jioni na mechi ikaanza saa 1 usiku.
    Mgeni alikuwa ni mke wa makamu wa rais, mama Aisha Bilal aliyeambatana na mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda.
    Michuano hiyo ilidhaminiwa na Serengeti Breweries Limited (SBL), Vodacom na Coca Cola pamoja na wadau wengine waliochangia kwa kuhamasishwa na Mama Tunu Pinda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA QUEENS YANG'ARA NETIBOLI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top