![]() |
| Rachel, enzi za uhai wake akiwa na mtoto Princess Asia Mahmoud |
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) kinaungana na familia na wanahabari wote nchini kuomboleza
kifo cha Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando ameiambia
BIN ZUBEIRY leo kwamba chama kimeshtushwa na taarifa za kifo cha Rachel
kilichotokea usiku wa kuamkia leo, hivyo wanatoa pole kwa familia yake,
waandishi wa habari za michezo na wafanyakazi wenzake wote, wasanii na
wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mdau mkubwa wa
michezo na burudani.
Alisema kutokana na msiba huo, chama
kinaandaa taratibu zake za kuwasilisha rambirambi kwa namna tulivyojiwekea,
kwani marehemu hadi mauti yanamkuta alikuwa mwanachama mtiifu wa TASWA. Hivyo
upo utaratibu kama mwenzetu akitangulia mbele ya haki namna gani tunatakiwa
tufanye.
“Lakini pia upo utaratibu mwingine nje ya
chama ambao utahusu mtu binafsi kuwasilisha michango ya rambirambi, ambapo
TASWA inawasiliana na wahariri wote wa habari za michezo wasaidie kukusanya
michango ya rambirambi kwenye vyombo vyao, ambayo wataiwasilisha kwa wajumbe wa
Kamati Maalum ya kusimamia jambo hili,”alisema.
Aliwataja Wajumbe hao ni Angela Msangi ambaye atakuwa Mratibu akisaidiwa na Mwani
Nyangasa, ambao watashirikiana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA,
George John ambaye ni Katibu Msaidizi wa TASWA, Grace Hoka na Alfred Lucas
ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. “Tunaomba ushirikiano wa wadau katika
kufanikisha jambo hili,”alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment