• HABARI MPYA

    Friday, May 11, 2012

    JB CHUPUCHUPU KUUAWA KWA AUNT EZEKIEL


    MCHEZA filamu anayetamba kwenye ‘game,’ Jacob Steven ‘JB’ (pichani) hivi karibuni alinusurika kuuawa na majambazi waliovamia Pub ya msanii mwenzake, Aunt Ezekiel iliyopo eneo liitwalo Gereji Mwananyamala jijini Dar.
    Akizungumza na gazeti la Ijumaa, JB alisema kuwa baada ya majambazi hao kuvamia katika pub hiyo saa 5.30 usiku, hakuwastukia kama walikuwa wahalifu bali alidhani ni wateja wa kawaida.
    “Mimi sikuwashitukia kama wale watu walikuwa majambazi, ila baada ya kutoa bastola na kutuamuru tulale chini na tutoe kila kitu nikajua kimenuka, nikatimua mbio ambazo sijawahi kukimbia licha ya mwili wangu huu,” alisema JB.
    Aliongeza kuwa, wakati akitimua mbio aliwasikia watu wakimuaru asimame lakini hakutii hadi alipofika Kituo cha daladala cha Komakoma ndipo alisimama na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru na kifo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JB CHUPUCHUPU KUUAWA KWA AUNT EZEKIEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top