• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2012

    VIERA AWAAMBIA ARSENAL; MNAMPOTEZA VAN PERSIE, WALCOTT NA WILSHERE PIA WATAONDOKA


    Arsenal's Robin van Persie
    MGUU NJE... Robin van Persie
    Last Updated: 18th May 2012

    PATRICK VIEIRA ameanzisha vita ya maneno na klabu yake ya zamani, Arsenal kwa kusema: Mnampoteza Robin van Persie — na litakuwa kosa letu.

    Mshambuliaji RVP anatakiwa na mabingwa Manchester City, ambako Vieira hivi sasa anafanya kazi na Ofisa Maendeleo ya Soka.
    Na gwiji huyo wa Gunners amemuonya kocha wake wa zamani, Arsene Wenger kwamba Theo Walcott na Jack Wilshere pia wataondoka ikiwa Arsenal itashindwa kumbakiza Mholanzi huyo.
    Van Persie amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa Emirates.
    Vieira alisema: “Ni moja ya mambo ambayo wangeyamaliza muda mrefu tu uliopita. Ni vigumu kuelewa.
    “Ni vigumu kweli kupata mchezaji wa kiwango cha ubora wa  Van Persie ukiwa umebaki mwaka mmoja kote duniani. Ni kujiweka matatani kwa kiasi kikubwa, kwa sababu wamewapoteza Samir Nasri na Cesc Fabregas mwaka jana.
    “Kama watampoteza Van Persie, itakuwa mzaha. Kwa Samir na Cesc, unaweza kusema, ‘Sawa, hao wawili wameondoka, lakini unafahamu Jack Wilshere na Van Persie bado wapo katika klabu’.
    “Lakini ikiwa Robin anaondoka, hiyo inamaanisha labda mwakani Theo Walcott, na mwaka unaofuata atakuwa Wilshere.”
    Vieira, ambaye ataendelea kuwa mchambuzi wa Televisheni ya ITV katika Euro 2012, alisema: “Nini muhimu kwa Robin ni anataka kushinda mataji. Arsenal inatakiwa kumuonyesha anaweza kufanya hivyo akiwa Arsenal.
    “Kitu kizuri kwao ni kumsainisha mkataba na kusajili wachezaji ambao watamuonyesha wapo katika kiwango chake.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIERA AWAAMBIA ARSENAL; MNAMPOTEZA VAN PERSIE, WALCOTT NA WILSHERE PIA WATAONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top