Last Updated: 18th May 2012
LIVERPOOL imehamishia ndoana zake kwa Pep Guardiola ikitaka arithi mikoba ya Kenny Dalglish aliyetupiwa virago.
Kocha aliyachia ngazi Barcelona, anaongoza katika orodha ya makocha wanaotafutwa Kop, wengine wakiwa nikocha wa Wigan, Roberto Martinez na wa Swansea, Brendan Rodgers.
Wamiliki wa Kop, kampuni ya Fenway Sports Group ya Marekani wamekubali nafasi ya kumtwaa Guardiola ni ndogo. Lakini wanafikiri itakuwa ni kosa kubwa kushindwa hata kuzungumza naye.
Guardiola ameondoka Barca akisema anahitaji kupumzika japo kwa mwaka mmoja atulie na familia yake.
Kocha wa Newcastle, Alan Pardew na kocha aliyetimuliwa Chelsea, Andre Villas-Boas pia wanatajwa kwenye orodha ya walimu wanaotakiwa Anfield.
Lakini kwa sasa anayepewa nafasi kubwa ni Martinez, ambaye Kop wamepewa ruhusa ya kuzungumza naye.
Mmiliki wa Wigan, Dave Whelan amesema: “Roberto aliuliza kama anaweza kuzungumza nao, akap;ewa ruhusa. Sasa tunasubiri kuona wataamua nini.
“Kama Liverpool wana nia kweli, tunaweza kumpoteza.”
Mtu ambaye anaweza kuwa wa kwanza kutua Anfield ni Mkurugenzi wa Michezo wa Juventus, Fabio Paratici, ambaye Liverpool inamtaka kwa ajili ya nafasi hiyo hiyo.
0 comments:
Post a Comment