UMOJA wa vijana wa Yanga kesho unatarajiwa
kufanya mkutano maalum kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu
klabu hiyo, mkutano ambao utafanyika makao makkuu ya klabu hiyo kuanzia saa
nane mchana, imefahamika. Mwenyekiti wa umoja huo, Bakili Makele aliwaambia
waandishi wa habari leo kwamba lengo la kufanya mkutano huo ambao aliuita ni wa
amani tu ni katika kujadili baadhi ya mambo ikiwemo mwendeo iliyouonyesha timu
yao kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara, pamoja na masuala mengi ambayo
yatailetea manufaa klabu hiyo katika siku za baadaye, kabla ya kuwasilisha kwa
uongozi. “Tumetema ubingwa, pia kupata aibu ya kipigo cha mabao 5-0 toka
Simba,sasa tunataka tufute aibu hii katika michuano ya Kagame kwa kutetea
ubingwa wetu, hivyo tunahitaji tupate kikosi imara kinyume na hapo
tunawezageuka kuwa sinema kwani sina imani kama kuna wachezaji watabaki au
la,”alisema. Hata hivyo, Makele aliongeza kuwa iwapo uongozi utawazuia kufanya
mkutano katika klabu hiyo wataamua la kufanya, huku akisema anaamini hilo
halitatokea kwani wao ni wanachama halali na wana haki ya kufanya mkutano
katika eneo hilo. Kauli hiyo ya Makele inafuatia hivi karibuni uongozi kuwazuia
wazee wa baraza la klabu hiyo kufanya mkutano wao uliokuwa maalum kwa ajili ya
kujadili masuala kama hayo, ambapo wazee hao wamekuwa katika msigano na
uongonzi wa Yanga chini ya Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga baada ya kumtaka
aachie ngazi kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo..
SOURCE: DINA ISMAIL
(mamapipiro.blogspot.com)




.png)
0 comments:
Post a Comment