Manchester City imesogea karibu kabisa ya
mfundo wa kumalizia Ligi Kuu ya Engald na kutangazwa mabingwa kwa mara ya
kwanza baada ya miaka 44, baada ya Yaya Toure kufunga mabao mawili na kuipatia
ushindi wa mabao 2-0 timu yake dhidi ya Newcastle United.
Kiungo huyo anayechezea pia timu ya taifa
ya The Ivory Coast alifanikiwa kumfunga mlinda mlango Tim Krull kwa mkwaju
maridadi wa kimo cha beberu zikiwa zimesalia dakika 20 kabla mpira kumalizika.
Baadae kidogo Yaya Toure akaongeza bao la
pili kwa mkwaju wa karibu huku muda nao ukiwa umewatupa mkono Newcastle.
Manchester City sasa wanafahamu fika iwapo
watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya QPR katika mechi ya kumalizia msimu, basi
watatangazwa moja kwa moja mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya kandanda ya England.
Ulikuwa ni mchezo murua hasa kwa Manchester
City wakiongozwa na nahodha wao Vincent Kompany safu ya ulinzi, huku David
Silva akitawala eneo la kiungo na umaliziaji uliofana wa Toure akishirikiana na
kikosi kizima wakihakikisha hawafanyi makosa kulikosa kombe msimu huu.
Ulikuwa uwanja huo huo wa Newcastle tarehe
11 mwezi wa Mei mwaka 1968 ambapo Manchester City walinyakua ubingwa wa ligi
kwa mara ya mwisho. Takriban miaka 44 baadae inaonekana historia ipo njiani
kujirudia huku klabu hiyo ikisogea mbele ya Manchester United ambao waliokuwa
wanaongoza ligi hiyo kwa muda mrefu.
Clint Dempsey akiwa amefunga bao lake la 23
msimu huu aliisaidia timu yake ya Fulham kupata ushindi murua wa mabao 2-1
dhidi ya Sunderland.
Dempsey alipachika bao kwa mkwaju wa
free-kick umbali wa yadi 25 na kuwa bao la pili lililoipatia ushindi Fulaham na
kuipaisha hadi nafasi ya nane ya msimamo wa Ligi.
Djibril Cisse akiingia mchezaji wa akiba
aliiongezea uhai dakika za mwisho timu yake ya Queens Park Rangers iepuka panga
la kushushwa daraja baada ya hatimaye kufanikiwa kuwalaza Stoke bao 1-0
walioonyesha ubishi katika uwanja wa Loftus Road.
Cisse akiwa amesahauliwa na walinzi wa
Stoke alipokea pasi ya Anton Ferdinand akiwa karibu na lango na akaweka mpira
kimiani na kuwasukuma Bolton chini yao na wao kujikwamua eneo la kushuka
daraja.
Thomas Sorensen mlinda mlango wa Stoke
awali aliwanyima nafasi za kufunga Taarabt na Cisse.
Lakini hali ingekuwa tofauti kama Cameron
Jerome wa Stoke angefanikiwa kupachika bao baada ya mkwaju wake kupiga nyavu
ndogo dakika za mapema.
Tottenham nao wamepoteza nafasi ya
kujisogeza hadi nafasi ya tatu wakati Aston Villa walipofanikiwa kupunguza hofu
yao ya kushuka daraja kwa timu hizo kugawana pointi moja baada ya kufungana bao
1-1.
Ciaran Clark alikuwa wa kwanza kuipatia
Villa bao kwa mkwaju alioufyatua kutoka yadi 25 uliomgonga mlinzi William
Gallas na kujaa wavuni.
Gareth Bale alinyimwa nafasi ya kupachika
bao na mlinda mlango wa Villa Shay Given aliyekuwa macho langoni lakini mlinzi
wa Spurs Danny Rose baadae alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa rafu mbaya dhidi
ya Alan Hutton.
Hata hivyo baadae Richard Dunne alimchezea
rafu Sandro ndani ya sanduku la hatari na Emmanuel Adebayor akasawazisha kwa
mkwaju wa penalti na hali iliyowabakisha nafasi ya nne nyuma ya Arsenal kwa
pointi moja tu.
Wolves nao walifanikiwa kufuta rekodi ya
kufungwa mechi ya 10 mfululizo nyumbani kwao baada ya kulazimisha sare ya
kutofungana dhidi ya Everton.
Everton walifanikiwa kumiliki mpira muda
mrefu wa kipindi cha kwanza huku Nikica Jelavic akipachika bao ambalo mwamuzi
alilikataa kutokana na mshambuliaji huyo kuwa ameotea na pia Steven Pienaar
naye alikosa nafasi nyingi za kufunga.
Wolves walijirekebisha kipindi cha pili
lakini Everton bado waliendelea kuwa hatari langoni mwao huku Jelavic akipoteza
nafasi nzuri ya kufunga.
Hata hivyo Wolves ambao wameshateremka
daraja walifanikiwa angalao kupata pointi moja ya kwanza kwenye uwanja wao
tangu tarehe 4 mwezi wa Desemba.
James Morrison akiingizwa kipindi cha pili
alifanikiwa kuisawazishia West Brom ambao tayari walikuwa wameshafungwa mabao
2-1 na Bolton waliokuwa wakihaha kujinasua eneo la kushushwa daraja.
Martin Petrov alikuwa wa kwanza kuipatia
bao Bolton kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 24 kufuatia rafu iliyochezwa
na Keith Andrews.
Bolton waliongoza kwa mabao 2-0 baada ya
Billy Jones wa West Brom kujifunga mwenyewe, lakini baadae Chris Brunt na
Morrison wakafanikiwa kusawazisha mabao yote
LINEUP, BOOKINGS (7) & SUBSTITUTIONS (6)
Newcastle United
- 26 Krul
- 02 Coloccini
- 03 Santon
- 06 Williamson
- 14 Perch Booked (Ferguson - 74' Booked )
- 04 Cabaye
- 10 Ben Arfa Booked (Sh Ameobi - 74' )
- 18 Gutierrez
- 24 Tiote Booked (R Taylor - 82' )
- 09 Cisse
- 19 Ba
Substitutes
- 35 Elliot
- 16 R Taylor
- 31 Ferguson
- 15 Gosling
- 22 Marveaux
- 25 Obertan
- 23 Sh Ameobi
Manchester City
- 25 Hart
- 04 Kompany
- 05 Zabaleta Booked
- 06 Lescott
- 22 Clichy
- 18 Barry Booked
- 19 Nasri (De Jong - 61' )
- 21 Silva (Richards - 86' )
- 42 Y Toure Booked
- 16 Aguero
- 32 Tevez (Dzeko - 70' )
Substitutes
- 30 Pantilimon
- 02 Richards
- 13 Kolarov
- 07 Milner
- 11 Johnson
- 34 De Jong
- 10 Dzeko
Ref: H Webb
Att: 52,389
0 comments:
Post a Comment